The Real World Sehemu Ya Sita
The Real World (Ulimwengu Halisi) Episode 06 Story: Olest Elton Ilipoishia... Mlangoni palikuwa na mlinzi anasinzia nikaamua kupita moja kwa moja ndani. Kabla sijaingia nikasikia nimeitwa. "We kijana unaenda wapi??" Nikistuka mwili hadi roho, kuckia hvy. Ila nilijikaza asije kugundua kuwa mimi si mhusika. Niliamua kumchimba mkwara. Olest: Hivi we mzee umechoka kazi? (Nlimuuliza kwa ukali sana hadi akaogapa) Mlinzi: Hapana nini tatzo? Olest: Inamana husikii kama mganga mkuu anakuita au unataka tuache kufanya shughuli za muhimu kwajili yako. Mlinzi: Hapana sija... Olest: Haraka, nenda unaitwa sasa hivi. Alipoondoka kwangu ikawa nafasi ya kuingia na kupekua. Nilipata ujasiri wa kupekua maiti moja hadi nyingine, hadi zilizokuwa kwenye mafriji. Lakini haikuwepo maiti yake. Nilianza kupata matumaini labda hajafa yawezekana kaamishwa hospitali. Wakati natoka nilimuona mtu kwa mbali kama mamaake. Nilimfatili...