The Real World Sehemu Ya Nne

The Real World(Ulimwengu Halisi)
Episode 04
Story By: Olest Elton

Nikikaa tayari kumkabili yule chatu mwenye hasira."Huhuhuhu..." joka lilicheka kwa mzaha. " Normak" Nilisema hivyo nikiwa nashusha pumzi, nilijua ni normak anafanya yote hayo. "Kumbe kwenye hatari ni mwepesi hivyo!?" Joka lilisema huku likiendelea kucheka. "Mshenzi we! " nakalitupa panga chini nikashuka kitandani nikakaa kwenye kiti, yule chatu alijiviringishataratibu, akaanza kupungua ukubwa hadi akabadilika kuwa Normak. "We umeingiaje humu ndani!?" Nlimuuliza , " Hamna mlango wala ukuta unaoweza kunizuia mimi kuingia kokote" alinijibu akakaa kitandani. Nikachukua ile karatasi iliokuwa mezani nikampa. " Mpaka nielewe maana ya kilicho andikwa ndio nita saini, hata ukija na sura ya simba siwezi kusaini huu mkataba. Aliichukua ile karatasi akaondoka nayo akiwa ananiangalia kwa jicho la kutoridhika. Hali ya chumba changu ilikuwa ni mbaya vitu vilikuwa vimevurugika kutokana na purukushani iliyotokea, lakini nikasikia mlango wangu unagongwa kwa nguvu "we olest! Olest! Umelala!?" Bibi aliniita. "Nipo macho" nilijibu... "We olest! Amka!?" Aliendelea kuita... "we bibi inamaana hunisikii au!?" Nilimjibu kwa sauti kubwa lakini hakusikia aliendelea kugonga. "Npo machooo" nilijibu kwa sauti ya juu sana. Ghafla nilistuka kujiona nimekaa kwenye kiti kichwa changu nimeegemeza kwenye meza nilipoinua kichwa niliona mazingira ya chumba changu yakiwa tofauti, chumba kilikuwa kimepangika vizuri kama nilivyokipanga wakati nilipoenda shule. Na hapa kuwa na mvurugano wa aina yoyote kama hakujatokea purukushani yoyote. "Inamana nilikuwa naota mda wote ule!?" Nilijiuliza... Nikweli ile ikikuwani ndoto tu hapakuwa na purukushani yoyote iliyotokea. "Bibi!" Niliita, "Unasemaje!?" Aliuliza."Ulikuwa unaniita?" Nilimuuliza... "Ndio nimeita weeee... nikajua haupo." Alinijibu, "aah nipo" niliamka nkatoka chumbani, kuangalia muda ilikuwainaelekea saa moja jioni. Sikuwa na kazi yoyote ya kufanya nkakaa na kuangalia Tv,ilipofika saa ya kulanilikula nikaenda kulala.Ilipofika jumatatu Asubuhi na mapema niliamka nakujiandaa nlivaa nguo zangu za shule nikajiangalia kwenye kioo changu kikubwa kilichopo chumbani. Nilijiona mimi lakini niliona taswira ya normak akiwa nyuma yangu, niligeuka nyuma sikumwona nikarudisha macho yangu kwenye kioo sikuiona ile taswira pia. Aaah nikapuuzia nikajua ni mawazo tu, nikaondoka zangu nikaenda shule, nilipofika shule tu kila mtu alikuwa ananisubiri kwa hamu " oya francy mbabe wako kaja" wapambe wakaanza kuchochea ili ugomvi utokee, niliongeza hatua zangu haraka haraka mpaka nikafika darasaninikaweka begi langu kwenye meza yangu kisha nikatoka nje. Kengele ya mstarini ikagonga tukajipanga kama kawaida. Safari hii aliinuliwa Francis kwaajil ya morning speech. Alipanda pale juu akaanza kujikanyaga kanyaga wanafunzi kwa walianza kucheka chini chini kwakuwa walikua waakimwogopa, mimi nilicheka kwa nguvu akanisikia akageuka akaniangalia vibaya, alishindwa kunifanya kitu sababu tulikuwa mstarini, tulipoingia darasani alikuwa akiniangalia kwa hamu sana. Nilimpotezea tukakaa darasani kumsubiri mwalimu wa somo lakini hakuja,ilikuja taarifa kapata dharula hivyo tujisomee kipindi chake. Kama unavyojua mda huo wanafunzi wakageuza viti na kuanza stori. Mimi kama kawaida yangu sinaga mtu wa kupiganae stori nikachukua kitabu changu cha history nikaanza kukisoma. Pembeni kunagroup la wanafunzi wa kiume wamekaa wakaanza kujadili mambo ya wasichana. Alex ndo alikuwa kama mwenyekiti wa kile kikundi maana alikuwa na stori kibao wenzie wakawa wamekaa kimya wana msikiliza , huyu jamaa alikuwa kama anasumaku kila msichana aliekua anamtaka alikuwa hamkatai na wasichana wengi walikuwa wanamfata na kumtongoza. Nilitamani nimuulize anatumia nini ila kutokana na jinsi nilivyo nikawa nashindwa. Alianza kuhadithia wenzie wasichana wa mtaani kwao aliotembea nao, akamaliza akaanza wa paleshuleni kuanzia Form I mpk Form III , akamaliza wenzie kwahamu wakawa wanasubiri awatajawatajie wa Form IV aliotembea nao. Maongezi yale yalinifanya kitabu kile nikiangalie kama picha mawazo na masikio yangu yote yalielekea kwao. Alianza kuwataja aliotembea nao mule darasani, akawa anahadithia na jinsi alivyokuwa anawafanya wakienda geto kwake, wapo waliokimbia,wapo waliosahau nguo zao za ndani,wapo walio zimia, wapo waliopiga makelele. Sehemu ilio nistua ni pale alipo mtaja Angel, moyo wangu nusu utokee mdomoni maana Angel ni msichana nlietokea kumpenda sana japo nilikuwa nnauhakika 100% kuwa sitoweza kuwa nae lakini nikishindwa kumpoteza ndani ya kichwa changu. "Yani huyu anavyo jilengesha mi nawapa siku mbili tu, mpaka jumatano au alhamisi huyu nakuwa nimesha mchapa, hii wiki hamalizi" alex alikuwa anawaambia wenzie aliongea kwa kujiaminisana. Hapo moyo kidogo ulitulia " kumbe bado hajapiga" nilijiwazia.Kiukweli mimi kila msichana nilie mjaribu alikuwa ananikataa tena kwa matusi, hakuna hata mmoja aliewahi kunijibu vizuri au kunikataa kistaarabu tu bila matusi. Hali hii ikafanya mimi kujitoa kabisa katika swala la mapenzi. Na mpaka wakati huu sikumjua msichana yoyote toka kuzaliwa. Hali iliyonishangazahata machangudoa walikuwa wakinikataa japo nilienda na hela nyingi sana. Niliwaza tatizo langu ni nini lakini kulikuwa hamna majibu,niliona maongezi yao yananichanganyatu nikaamua kulala juu ya dawati langu,. Baada ya muda kengele ya mapumziko iligonga , wanafunzi walitoka na mimi nilitoka nkaelekea kwenye kununua vitu kama ilivyo kawaida ya wanafunzi wakati wa mapumziko. Nilipofika kwenye ngazi tu yalile jengo nikakumbuka kuwa kuna mtu alikuwa ananiwinda, na alikuwa tayari kesha niona. Niliwaza nirudi nilikotoka au niingie, niliona nikirudi nyuma ntaonekana dhaifu, nikaingia kibishi tu. Nikanunua vitu vyangu nikaweka kwenye mfuko, wakati na nunua vitu nikasikie sauti za upambe za chinichini"enheee.... haya sasa.... mwenyeww huyoo" nilivyosikia hivyo nikaanza kununua vitu haraka haraka ili niondoke kabla ya lolote kutokea. Francis ali kuja akasogea kidogo tukawa tumeachana nae kama umbali wa hatua tano. "We boya! Leo ndo iwe mara yako ya kwanza na yamwisho kuja eneo hili" aliniambia kibabe. Nilikumbuka kuwa normak anahitaji msaada wangu hivyo hatari yoyote itakayo nikabili atanisaidia, baada ya kuwaza hilo nikapata ujasiri. "Kwani jengo la baba yako hili!? Kama unaona mimi nafaidi sana kuja hapa libebe basi hili jengo kampelekee mamaako" nilimjibu kwa jeuri."Haaaaaaa......" wanafunzi wote mle ndani walishangaa wapi nimepata kiburi cha kumjibu mbabe wa shule. Francis alivua shati akamkabidhi mpambe wake "leo unatoka maiti humu ndani" aliniambia akiwa kajawa na hasira. Nikaanza kuuhisi uwepo wa Normak, nikapata ujasiri nikajua ni lazima atanisaidia tu. Wala sikutaka kugeuka kumwangalia yuko wapi nilianza kumhisi kila alipotua.

Itaendelea

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Madam Lilly Sehemu Ya Pili

Madam Lilly Sehemu Ya Tano

Madam Lilly Sehemu Ya Tatu