The Real World Sehemu Ya Tano

The Real World (Ulimwengu Halisi)
Episode 05
Story: Olest Elton

Ilipoishia....
      Nikaanza kuuhisi uwepo wa Normak, nikapata ujasiri nikajua ni lazima atanisaidia tu. Wala sikutaka kugeuka kumwangalia yuko wapi nilianza kumhisi kila alipotua.

    Hapo nilipata ujasiri wa kupambana nae japo alikuwa n mbabe. Waliotuzunguuka walikaa tayar kwa kushuhudia pambano,ambalo walikuwa wakilingoja kwa hamu. Aliporusha ngumi niliinama haraka, japo mwili wangu ni mnene ila nilikuwa mwepesi ningeweza kukwepa hata risasi. Alijaribu ngumi ya pili,alipopiga kushoto mimi nikaelekea kulia akanikosa pia. Mpaka wakati huo mimi wala sikufanya shambulizi lolote. Kabla hajafanya shambulizi jingine nilimgusa kidogo tu kifuani alienda kuangukia kwenye vitumbua vya watu. Kitendo kile kilimwacha kila mtu mdomo wazi. Niliamua kuondoka. Wakati natoka nilimeona Angel hatua chache mbele yangu akiwa anaelekea nakotoka. Ghafla! Nilihisi kunakitu ninakuja kwa kasi,haraka nikainama. Lilinipita jiwe kubwa ambalo moja kwa moja lienda kumpiga Angel tumboni. Alianguka pale chini na kugala gala kwa maumivu. Kila mtu alishuhudia lile tukio. Angel alikuwa hoi akitoa dam mdomoni. Nilimbeba nikaanza kukimbia kuelekea hospitali. Mwalim alikuja akamchukua francis na kwenda nae ofisini akatoe maelezo. Nilifika hospitali nikapokelewa na madaktari nikatoa maelezo,nikaambiwa nirudi nikawaite wazazi wake. Nilipokuwa njiani narudi shuleni,nilipishana na wazazi wawil wakiwa wanakimbia wanaonekana na haraka. Nlikuwa nisha changanyikiwa sikuwatilia maanani.
    Nlipo fika shule ilikuwa ni kesi kubwa mambo yote yalinigeukia mimi. Nilijua sina makosa ila kutokana na tatzo langu la kuchukiwa na watu ndo lilisababisha. Mwalimu alitaka kutusimamisha wote shule. Aliandika barua ya kutusimamisha sote wawili,kabla hajatukabidhi barua tuondoke normak alitokea nyuma yake. Alimgusa kichwa kisha akasema.
Normak: "mmmh!!! Ila hapana  wewe francis ndo unamatatizo sana. Wewe ndo ntakusimamisha shule kwa muda wa mwezi mzima. Na siku yakuja shule uje na mzazi."(Mwalim nae alirudia maneno ya normak vile vile kama alivyo yasema.)
Fransic alipewa barua. Barua yangu ilichanwa na kutupwa kwnye kindoo cha taka, nikAruhusiwa kurudi darasani. Nilikaa darasani nikiwa sina amani mawazi yot yalikua hospital kwa Angel. Tulipo ruhusiwa nilienda hospitali. Nilipofika nilizuiliwa nikaambiwa sio muda wa kuona wagonjwa. Nilirudi nyumbani, nikijaribu kumwita normak lakini hakutokea tena. Nilirudi hospitali, nikaingia kwa njia za panya. Nje ya wodi nilimwona mama mmoja ambae kafanana na Angel,bila shaka alikuwa ni mamaake alikuwa akiongea na daktari. Nilitamani kujua nini wanachoongea ila nilikuwa mbali sana sikuweza kuwasikia. Niliamua kuwaangalia mijongeo ya midomo yao kwa makini kujua wanaongea nini. Nilimwangalia daktari midomo yake kwa makini nikagundua kuwa alikuwa anasema.
Daktari: Tunafanya kila tunaloliweza kuokoa maisha ya mgojwa wako mama. Lakini kiukweli hali sio nzuri kabisa Kaumia sana kwa ndani anavuja dam na ........

Sikutaka tena kujua daktari alikuwa anataka kusema nini. Niliamua kuondoka nikiwa nimewaacha wakiendelea na mazungumzo.
Nilirudi nyumbani nikajifungia chumbani kwangu nikiwa najilaumu kwann niliamua kupigana,kama ningeondoka eneo lile yote yasinge tokea. Siku hyo hata normak hakunisumbua tena hata ndotoni. Kesho yake sikwenda shule,niliamkia hospitali. Nilienda wodi aliyokuwa amelazwa Angel ili nikamuone. Moyo wang ulipasuka nilipoona kitanda alicholazwa Angel kikiwa kina tandikwa hakina mtu tena. Nilitaka nianze kushusha kilio ila nilikausha kwanza mi mtoto wa kiume sikutaka kuleta vihoja. Sikutaka kuanza kuomboleza bila kuhakikisha kama yupo hai au kafa. Hivyo nilienda wodi iliyofuata lakin haiuwepo,nilienda iliyofuatia pia hakuwepo. Nilienda hadi wodi ambazo asingeweza kulazwa kama vile wodi ya wajawazito, vichaa kote huko niliktafuta. Hapo basi moyo wangu wote ulikubali kuwa amekufa. Ila nilitaka kuiona maiti yake ili kuhakikisha. Hivy nilirudi nyuma nikaingia maabara nikakuta kuna makoti yametundikwa  nikachukua moja nika vaa, kisha nikashuka kwenye chumba cha maiti. Mlangoni palikuwa na mlinzi anasinzia nikaamua kupita moja kwa moja ndani. Kabla sijaingia nikasikia nimeitwa.  "We kijana unaenda wapi??"    Nikistuka mwili hadi roho, kuckia hvy.

Itaendelea.....

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Madam Lilly Sehemu Ya Pili

Madam Lilly Sehemu Ya Tano

Madam Lilly Sehemu Ya Tatu