The Real World Sehemu Ya Tatu
The Real World(Ulimwengu Halisi)
Episode 03
Story by:Olest Elton
Nilimwangalia normak na yeye alikuwa akiniangalia mimi. Wanafunzi wote walinishangaa maana hawakuona nlichokuwa nakiangalia, nligeuka pembeni nlikutana na Angel macho kwa macho kisha nikageuka haraka normak alikuwa kashapotea, nlijibaraguza kisha nikaendelea na historia nliokuwa nawaelezea, nkaamua kuifupisha iki niondoke kabla sijapata matatizo mengine. Nikamaliza kisha nikarudi kujipanga mstarini. Tukaamrishwa kuingia madarasani wakati naenda darasani nikakutana na madam wa history akanipa pole, lakini pole yake alionipa ni kama mtu aliotoa tu ili kutimiza wajibu sio ile ya kuonesha ameguswa na tatizo langu. Nami niliipokea tu. Sikudhani kama sikumoja maisha yangu yangekuwa kama kasuku kwenye kundi la kunguru, nikakosa hata wa kunipa salamu. Uwepo wangu ulikuwa ni kero kwa kila aliyeniona. Niliwaza ni kwanini? Ila sikupata jibu. Sikuwa na muonekano mzuri wa kuvutia ila walikuwepo wabaya kuliko mimi ila walikuwa na marafiki tena wengine walikuwa mpaka na wapenzi. Nlitamani hata rafiki kwa sekunde moja tu nijue ladha ya rafiki ikoje. Ila kilio changu kilikuwa ni kama cha samaki machozi kwenda na maji. Nilikaa kwenye meza yangu nikafungua begi langu kutoa kitabu peni ikaanguka chini, nilipo inama kuiokota nikaona chini ya meza yangu maandishi yasiyo eleweka 未曾幾何時我想座椅不會 .... Nilikereka sana, maana yale maandishi yalinikumbusha mkataba. Kitu ambacho nilikuwa nimekwisha aanza kukisahau. Nilikaa nikaegemeza kichwa juu ya begi langu lililokuwa juu ya meza. Masomo yaliendelea hadi ilipofika muda wa mapumziko,kama kawaida yangu nikiwa sina hela huwa nakaa nyuma ya darasa natulia kipeke yangu peke yangu. Niliegemea ukuta huku nimefumbata mikono kifuani mwangu, nilihisi nimegusa kitu km karatasi kwenye mfuko wangu wa shati. Niliangalia ilikuwa ni hela sh.5000 mh! Nilijaribu kuvuta kumbukumbu kama ile hela ni yakwangu na niliiweka lini lakini akili haikunipa kabisa. " Kwanini usiende kuitumia hiyo hela badala ya kujiuliza inatoka wapi" sauti ilisema.. Moja kwa moja nilijua nani aliyesema hivyo " Normak! Asante, ila hata unipe nini siwezi kusaini mkataba nisio ujua"nilisema nikiwa nimeinamisha kichwa changu chini. Sikusubiri majibu yoyote niondoka na ile hela nikaelekea sehemu ambayo wanafunzi wananunua vyakula mbalimbali,nilimuona Angel pia akiwa na wanafunzi wengine akinunua chakula. Nilipo ingia ndani ya lile jengo ili kununua chakula sauti za watu zilianza kushuka chini hadi kukawa kimya kabisa, mimi mwenyewe nikaanza kujistukia labda uwepo wangu ndo unasababisha yote hayo. Ila sikujali nikaenda kwa mmoja wa wamama wanao uza vitu aliyekuwa karibu na mlango wa nyuma wa jengo lile.Wakati na nunua vitu alisimama mbabe wa shule francis "Ouya we ms*ng* fanya fasta usepe unatuwekea kiwingu" aliongea kibabe. Kutokana na ukimya wa watu sauti ile iliskika sana na kila mtu aliisikia. "Ms**ng# baba yako! Kama unataka uhuru nenda kale kwa mamaako" nilimjibu ili nisionekane mdhaifu, lakini moyoni nilikuwa naogopa sana,niliogopa zaidi nilipo waza nini kitatokea baadaya kumjibu vile.. " haaaaaaaa.....!Jamani.... eeeh... yani na wewe unakubali, " " haaa... yani ingekuwa mimi....." " duhh... mimi sikubali aisee...." sauti za wapambe wa francis na wanafunzi wengine. Wanafunzi wote walitamani kuona ninavyo pokea kichapo ili wafurahi. "Ah! Umekuwa mbabe sikuhizi eeh..! " aliniambia francis huku akijongea taratibu kama simba anaemyemelea swala. Mkononi mwake alishika bakuli lilokuwa na mchuzi akanirushia, niliinua mkono ili kujikinga lile bakuli lisinipige. Lile bakuli lilipofika karibu na mkono wangu likaanguka chini bila hata kunigusa,kitu kilicho washangaza wengi ni kwamba bakuli lilikuja kwa kazi lakini lilianguka bila hata kunigusa , pia lilituachini bila kuvunjika japokuwa lilikuwa ni bakuli la udongo. Mimi pia nilishangaa nguvu hiyo nimeitoa wapi. Niligeuka kuangalia mlango wa nyuma, kwambali nilimuona Normak aliwa kanyoosha mkono kama mimi nilivyofanya wakati wa kujikinga. Moja kwa moja nilijua kuwa si mimi niliefanya kitendo kile, alikuwa ni Normak. Francis alibaki kasimama wala hakunisogelea, nilienda kwa yule mama nikachukua vitu vyangu nikaviweka katika mfuko wa rambo nikachukua hela iiyobaki kisha nikaondoka kuelekea darasani. Nilipofika nikafungua mfuko na kuanza kula vile nilivyonunua, wapo waliokuwa hawana helana.wenye njaa lakini sikuwahi kuombwa chochote na mtu yoyoye. Nilitamani kushea vyangu na watu lakini nilishindwa kutokana na kila mtu kutonipenda,ilinibidi nizoee mazingira ya kipeke yangu. Siku hiyo nilifanikiwa kusoma vizuri bila tatizo lolote la kuanguka wala kujisikia vibaya. Nilirudi nyumbani moja kwa moja nikaingia chumbani kwangu, nikavua shati tu,kisha nikakaa kwenye meza ya computer ,pembeni ya meza kulikuwa na karatasi nlipoifunua nlikutana na ule mkataba wa maandishi yasiyoeleweka, nilikereka sana nakaufunika ule mkataba.Ghafla nilisikia kama kunakitu chini ya uvungu wa kitanda kinataka kutoka ,sikuinama kuchungulia ila nilisubiri kuona ni kitugani. Mara kilijitokeza kichwa cha Chatu mkubwa sana mweusi, nilistuka nikapanda juu ya meza aliendelea kutoka taratiiibu hadi mwisho. Akasimamisha kichwa chake, alisimama hadi akalingana urefu na mimi. Nilishindwa kupiga kelele nilishindwa kukimbia nilibaki nimesimama tu juu ya meza, alisogea hadi karibu na uso wangu tukawa tunaangaliana macho kwa macho. Yule nyoka alijaa robo tatu ya chumba kizima,jasho lilinitoka nikishindwa nifanye nini, nalenyewe lilibaki linaniangalia. Lilipozidi kujisogezakwangu,mkia wake uligisa chupa ya soda ilakaanguka, ile kelele ililisitua likageuka nyuma kuangalia. Kwa kitendo kile sikupoteza hata sekundenikaruka upande wa pili kwenye kitanda pembezoni mwa ukuta nikatoa panga,nilipo heuza shingo liikutana na upanga, nililichana mara mbili lakini ngozi yake ilikuwa ngumu sikufanikiwa kulikata kichwa ila nililijeruhi tu, ilkuwa ni kama nimetia chumvi kwenye kidonda. Ilipiga kelele ya hasira likazidi kutuna na likakaa tayari kwajili ya kunishambulia. Liliinua kichwa kikakaribiana na dari,nami nikashika upanga wangu vizuri nikisubiri kuona litakuja kwa namna gani.
Itaendelea
Maoni
Chapisha Maoni