The Real World Sehemu Ya Pili
The Real World(Ulimwengu halisi)
Episode 2
Story by: Olest Elton
0684037884
Niliangalia mlangoni ila hapakukua na mtu yoyote alieniita. "Olest" aliniita mwalim, "yes madam" niliitika. "Endelea" alinitaka niendelee. Niliendelea kuelezea ila ghafla nikaona hali yangu inaanza kubadilika. Niliona moyo wangu unaenda mbio sana,nilijikaza nkaendelea kutoa somo lakini nikaona kifua kimeanza kunibana, nkawa nashindwa kuvuta pumzi nlianza kupepesuka kisha nikaanguka chini. Na sikuelewa kilicho endelea baada ya hapo. Nilionagiza tu, giza totoro. Nilijikuta nimekaa kwenye kiti kichwa changu nimelaza juu ya meza yangu ya nyumbani ya kusomea,lakini ilikuwa ni katikati ya msitu mzito. Kulikuwa ni kimya sana kimya kilitandahadi nilikuwa nikijisikia mapigo yangu ya moyo yanavyoenda. "Olest" sauti ikiita tena nikageka nyuma sikuona mtu. Nilipo sudisha uso wangu mbele nilikutana uso kwa uso na mtu nisiye mfaham,nilistuka maana sikujua amefikaje na saa ngapi amefika. Ila sura yake na macho yake hayakuoneshauovu wa anina yoyote, nilipo mwangalia usoni jina lake lilinijia kichwani bila kuambiwa "Normak" ..."We ni nani?" Nilimuuliza, "Hahahahaha" alicheka taratibu kwa pozi zote. "Kwanini unaniuliza wakati tayari umekwisha nijua?" ... Nilishangaa ajuaje kamanimemjua "Unataka nini?" Nilimuuliza nikiwa makini sana kujua nini anataka. "Nlikuwa nausubiri huu wakati kwa muda mrefu sana, nimekua nakusubiria toka hujazaliwa, nmekuangalia kuzaliwa kwako mpaka hivi ulivyo sasa" alinambia kwa sauti ya chini. Nilisimama "We ninani?" Nilimuuliza nkiwa.nmekuja sura. "Hilo sio la muhimu sana , utalijua wakati ukifika. Cha msingi ni mimi ninataka nini" alinijibu bila wasiwasi wowote. Kiukweli nilikuwa sijamwelewa anachoongea na wala nlikuwasijaelewa nipo wapi "unataka nini, na hapa nipo wapi" nilimuuliza ndani ya moyo wangu nikiwa nina wasiwasi sana. "Hapa upo kwenye ulimwengu halisi.Nia ya kukuleta hapa ni kutaka kusaini mkataba na wewe" alinambia huku akiniangalia machoni."Ulimwengu halisi!??? Ndo wapi?? Nahuo ni mkatabagani?? Nlimuuliza nikiwa.na mshangao mkubwa. " Utajua mengi wakati ukifika" alihitimisha hivyo kiufupi kisha akaweka karatasi mezani "Huu ndio mkataba naotaka usaini" alinambia akiwa anasubiri ni saini. Niliuchukua ule mkataba na kuusoma lakini sikuelewa lugha ilo tumika, 勃箈崔的士站他鄉鎮壓畋!不要緊迫使臣子曰:這回應急速效應變之所以我認為你家中間商店長達能源源不絕不過了!還在乎乾啦是否 baada ya.kuona maandishi ya aina hii akili ikinijia kuwa yale maandishi niliyaona shule. Nilijua ile itakuwa ni ndoto maana nilianguka shuleni. "Sijazi mkataba nisio uelwa, nirudishe nilikotoka" nilisogea pembeni ya.kiti na ile meza."Siwezi2 kufanya hivyo hadi ujaze mkataba" alinisisitiza. "Ntajirudisha mwenyewe" nilimjibu hukunkaanza kujipiga makofi kichwani ili kama ni ndoto niamke. "Unajisumbua olest unadhani kama ingekuwa............." kabla hajamalizia kusema alichokuwa anataka kusema mimi nilipiga kelele kwa hasira kutoka chini ya uvungu wa moyo kwa nguvuuzangu zote" Wake uppppppp"...Nilizinduka nikiwa kwenye kitanda cha hospitali nikiwa nimetundikiwa maji. Nilihisi mwili wangu ulikua na nguvu wala sikuwa mchovu hivyo niliamkana kuanza kuchomoja drip waliokuwa wamenitundikia nlipotoka nje nlikutana nanesi alikuwa akija kwenye wodi nlio lazwa, "hee! Nan kakuruhusu kutoka? Rudi bado unaumwa." Alisema hivyo akanishika mkono anirudishe wodini. Nlichomoa mkono wangu"Mi najisikia vizuri wacha nirudi nyumbani saa hizi" nili mjibu huku naondoka. Nesi aliita.manesi na madokta.wenginewakanikamata wakanizuia kutoka. Sikutaka kuleta vurugu maana ningeonekana kama mgonjwa wa akili. Walinirudisha wodini wakakuta nmejichomoa drip. Walinipeleka kwa daktari alie nipokea. Alinitazama na kuona hali yangu nipo vizuri, alishangaa sana. Niliangalia saa ya ukutan ikikuwa ni saa 8 mchana "Haa! Kuzimia masaa matatu tu ndo mnakuwa na wasiwasi hivyo?" Nikiuliza nikijua ni masaa matatu toka nilipo patwa na tatzo lile, maana shuleni nilijisikia vbaya na kuanguka kwenye mda kama saa4 au saa 5 hivi asubuhi. Dotka na wale manesi waliangaliana wakanishangaa.."vipi?" Niliuliza... "unajua leo ni lini?" Niulizwa na dokta"aaammmm.. leo... niiii... jumatatu" nlijibu. Dokta alinipa simu yake nikaangalia sikuamini macho yangu ikikuwa ni alhamis. Siku tatu nzima nilikuwa sina fahamu. Niliamua kuamka na kuondoka, walipotaka kunizuia niliponyoka nkakimbia.Nilifika hadi nyumbani nkamkuta bibi akiandaa uji aniletee hospitali. Aliponiona alistuka pia akafurahi sana akanikumbatia akiwa haamini macho yake."Hee! Wewe ilikuwaje huko shule?" Aliniuliza "Tatizo langu la siku zote" nilimjibu. Alishindwa kuongea alibaki akiniangalia kwa jicho la huruma. Niliingia chumbani kwangu. Nikachukua taulo nikaenda kuoga, kisha nkabadlisha nguo. Nikakaa kwenye computer ya chumbani kwangu nikaanza kupekua vitu mbali mbali kwenye mtandao. Kiukweli tulikuwa tunaishi maisha mazuri japo hatukuwa matajiri pia hatukuwa masikini, tulikuwa ni wa maisha ya uwezo wa kati. Baadae nilikaa kitandani nikaanza kufikiria nlichokua naambiawa na normak. Pia niliwaza sana juu ya matatizo niliokuwa nayo.Asubuhi ilipofika nilienda shule nlipofika shuleni watu walianza kunishangaa,kila mtu alinikodolea macho "We ungemalizia wiki nyumbani, ijumaa unakuja.kufanyanini!?" Mwanafunzi mmoja nnaesomanae aliropoka. Wote walio sikia walicheka.Sikujali niliendelea kwenda,nlipofika.darasani niliweka begi langu juu ya meza yangu. Kisha nkatoka nje. Baada ya dakika chache kengele ya mstarini ililia. Wanafunzi wote walijipanga kwenye mistari yao, tukaimba uwimbo wa taifa kisha uwimbo wa shule. Ulifika.wakati wa matangazo alisimama kiranja wa taaluma akasema" morning school, now its morning speech time, starting with Olest Elton". Nlistuka maana ilikuwa na wala.sikupewa muda wa kuiandaa speech. Nilijipa moyo nikaenda kusimama kati kati ya wanafunzi wote wakiwa wamenyamaza kimya wananisikiliza nini ntaongea, na wengine kuangalia kama ntaanguka kuzimia au vipi. Nlianza kwa kuwasalimia wanafunzi, kisha nikamshukuru kiranja wa taaluma kwa kunipa nafasi ile. Nlianza kuongelea historia fupi ya dikteta Joseph Stalin nilielezea nikiwa nime relax maana nlikuwa nikiijua vizuri. Wakati naendelea kuelezea mbele yangu alitokea mzee Normak. Nikanyamaza kwa muda nkabaki namshangaa...
Itaendelea.
Maoni
Chapisha Maoni