The Real World

The Real World(Ulimwengu Halisi)
Episode1
Story By: Olest Elton

Ilikuwa ni wakati wa mapumziko nilikuwa nimekaa nyuma ya darasa. Nilikuwa nimekaa peke yangu maana sikuwa na rafiki yoyote pale shuleni, nilikuwamimi kama mimi. Ni miaka mi nne sasa toka nmeanza kidato cha kwanza hadi nimefika kidato cha nne lakini sikuwahi kuwa na rafiki japo nilikuwa sio mgomvi wala mwenye majivuno lakini hakuna mtu aliependa urafiki na mimi, kila nilipo jaribu kuwamkarimu na mcheshi na kila nlipoongea na watu walinihama. Hali hii ilinipa wakati mgumu sana pale shuleni. Ukizingatia nlikuwa na tatizo la kubanwa nakifua pia nilikuwa ni mtu wa kuanguka anguka kila wakati na kupoteza fahamu kila wakati hivyo nilihitaji uangalizi wa kutosha. Nili hangaika vituo mbali mbali vya afya kujua nini tatizo langu lakini halikuonekana. Hali hii ilifanya maisha yangu kuwa magumu sana hasa katika swala la taaluma. Nlipo kuwa nmekaa peke yangu kimya bila kusemeshwa wala kumsemesha mtu yoyote alipita mwanafunzi wa kike mbele yangu alikuwa anaitwa happy."Mambo vipi?" Nlimsalimia nkiwa nimeweka tabasam katika uso wangu, (hakuitika alinisonya akaenda zake) .... "hahahahahaha... " nilicheka tu wala haikuniuma maana hii ilikuwa ni hali ya kawaida tu miaka yote mi nne hapo shuleni ilikuwa ni hivyo sikupendwa na mtu wa aina yoyote hata salam yangu ilikuwa haipokelewi.Kengele ya kuingia darasani ililia niliingia darasani kuendelea na masomo. Dakika 10 Baada ya kengele kulia aliingia mwalimu wa history darasani kwetu akiwa ameongozana na binti mmoja aliekuwa amevaa uniform zisizokuwa za shule yetu. Mwalimu alisimama mbele yetu na yule binti na kumtambulisha , jina lake alikuwa anaitwa Angel alikuwa ni mweupe sana mrefu, pia alikuwa amejaaliwa umbo wanafunzi kibao walimtolea macho pale darasani. Kiufupi nilivyo muona nilimpenda sana ila sikutaka kushoboka kwa sababutatizo langu ninalijua.Mwalimu alimruhusu achukue kiti akae, alikuja akakaa dawati lilokuwa karibu na mimi. Nlihisi joto limeongezeka nlikuwa naogopa hata kugeuka nyuma kumwangalia. Mwalimu alianza kutufundishahistory alitufundisha mada ya vita ya kwanza ya dunia tulikuwa tumefika kwenye kipengele ya Great Depression. Hiyo sehemu nilikuwa nimekwisha isoma tayari nlipokuwa nyumbani, nkaona kama mwalimu ananipotezea muda tu. Hivyo nikaamua kulala juu ya meza yangu. "Olest" mwalimu aliniita"Naam.." nikiitika. "Simama" aliniamuru , bila kubisha nilisimama. "Njoo hapa" aliniita niende mbele ya darasa. Nilisonga taratibu mpaka nilipo fika pale mbele. Alinipa kitabu cha history ambacho ni oxford,kisha akaniambia niwasomee subtopic ya Great Depression mpaka mwisho kisha nielezee. Wala sikuogopa maana nlikuwa nishasoma ile sehemu kabla. Pia nkaona ile ndo nafasi nzuri ya kuweka swagga ii nimshangaze mtoto mzuri ale kuja.Nilifungua kile kitabu kisha nikafunua sehem nilio ambiwa nikaanza kusoma kicha cha habari " The Great Depression of 1929-1933" baada ya hapo nkaooona machozi yamenilenga nkawa sioni vizuri. Nlichukua kitambaa nkajifuta Mara baada ya kujifutaniliona maandishi yamebadilika...还真实性子孙你是哦了,好朋友!我还没见 nlishangaa imekuwaje Nlianza kuona lugha nisizozielewa, nilitumbua macho kama fundi saa lakini sikuelewa chochote. Nliinua macho yangu yakakutana moja kwa moja na Angel niligeuka haraka mwalim akawa ananiangalia, wanafunzi wakaanza kunong'ona chinichini. Nkaangalia kile kitabu tena nikaona maandishi yanadondoka kutoka kwenye kitabu hadi chini, herufi moja moja zilianguka hadi kitabu kikabaki kitupu. Niliangalia chini ila yale maandishi siku yaona,wote walibaki wananishangaa mimi. Nilikifunga kile kitabu nikainua kichwa changu kisha nikatabasamu. Nikampatia mwalimu kitabu chake nikaweka mikonoyangu mfukoni kwa mbwebwe. Ilibidi nitoe vitu kutoka kichwani maana ile sehemu niliisoma nlipokuwa nyumbani nikaielewa vizuri, pia niliimeza yote kichwani kama ilivyo. " Alright students Today we gonna.discuss about The Great Depression of 1929 - 1933 " nilisema hivyo kwa kujiamini kisha nikachukua chaki na kuanza kuwaelekeza. Wakati nawaelezea nikisikia sauti iliyo nong'ona kwa ukali"Olest" niligeuka kuelekea mlangoni kulikuwa hamna mtu

Itaendelea....

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Madam Lilly Sehemu Ya Pili

Madam Lilly Sehemu Ya Tano

Madam Lilly Sehemu Ya Tatu