The Real World Sehemu Ya Sita
The Real World (Ulimwengu Halisi)
Episode 06
Story: Olest Elton
Ilipoishia...
Mlangoni palikuwa na mlinzi anasinzia nikaamua kupita moja kwa moja ndani. Kabla sijaingia nikasikia nimeitwa. "We kijana unaenda wapi??" Nikistuka mwili hadi roho, kuckia hvy.
Ila nilijikaza asije kugundua kuwa mimi si mhusika. Niliamua kumchimba mkwara.
Olest: Hivi we mzee umechoka kazi? (Nlimuuliza kwa ukali sana hadi akaogapa)
Mlinzi: Hapana nini tatzo?
Olest: Inamana husikii kama mganga mkuu anakuita au unataka tuache kufanya shughuli za muhimu kwajili yako.
Mlinzi: Hapana sija...
Olest: Haraka, nenda unaitwa sasa hivi.
Alipoondoka kwangu ikawa nafasi ya kuingia na kupekua. Nilipata ujasiri wa kupekua maiti moja hadi nyingine, hadi zilizokuwa kwenye mafriji. Lakini haikuwepo maiti yake.
Nilianza kupata matumaini labda hajafa yawezekana kaamishwa hospitali. Wakati natoka nilimuona mtu kwa mbali kama mamaake. Nilimfatilia hadi nilipoingia kwenye wodi za watu mahututi. Nilijiona mjinga sana. Kuhangaika kote kule nilishindwa kufikiria kuwa kunawodi za watu mahututi. Ila bado nilikuwa na wasi wasi mkubwa juu ya hali ya Angel. Kama hadi kapelekwa ICU (Intensive Care Unity) inamaana hali haikuwa nzuri kabisa. Nilirudi nyumbani.
Nilikuwa nimechoka nikataka nipumzike kidogo. Nilienda kitandani nikajilaza,taratibu kikaja kiusingizi kikanipitia. Nikaanza kujihisi kama nimekaa tofauti. Nilifumbua macho nikajikuta nimekaa kwenye mabenchi ya hospitali. Kabla sijakaa vzur kujiuliza nimefikaje alikuja daktari.
Daktari: ooh! We ni rafiki yake na Angel.
Olest: e...eeh..e.!! Ndio ( nilijibu bado nikiwa aijielewi vizur)
Daktari: Nifate basi ofisini.
Nilimfata ofisini huku akili ikijiuliza kuwa nimefikaje wakati nilikuwa nyumbani nimelala??. Daktari aliingia ofisini akaketi kisha akatoa makaratasi kwenye droo yake.
Daktari: Sasa kijana, tunataka kwenda kumfanyia oparesheni Angel kabla hali haijawa mbaya zaidi. Kwa hyo kabla hatujamfanyia upasuaji huo,tunahitaji usaini karatasi hizo.
(Nilishangaa)
Olest: Kwanini nisaini hizi karatasi.!!!??
Daktari: Tunaoenda kufanya hii kazi ni binadamu, na yamungu ni mengi. Inabidi usaini kwajili ya usalama wetu. Kama lolote litatokea sisi hatuta husika.
(Nilishangaa hata zaidi)
Olest: Kwanini mimi nisaini wakati mimi sio ndugu, mi ni mwanafunzi mwenzie tu.
Daktari: Hakuna ndugu yake wala mtu mwingine wa karibu alie jitokeza hadi saa hizi.
Olest: sawa lakini huo ndo utaratibu wa wapi na umeanza lini?
Daktari: Nimechoshwa na maswali yako. Hatutomfanyia upasuaji. Tutasubiri lolote litakalotokea litokee. Usitulaumu.
( Baada ya kusikia vile nikiamua tu kukubali kusaini.)
Olest: Nipe basi nisaini.
Alinipa zile karatasi,nikatafuta sehemu ya kusaini.
Olest: Naomba peni tafadhari.
Daktari: huwa hatusaini na peni.
(Huo kwangu ulikuwa ni mshangao mwingine)
Olest: ntasainije sasa?
Daktari: nipe mkono wako.
Sikuwa na ahaka nilijua anataka kuchovya kidole changu kwenye wino. Lakin haikua hivyo. Nikivyo mpa kidole changu, haraka alinichana na damu yangu kugusisha pale kwenye mstari wa kuweka sahihi.
Olest: hiyo staili ya kusaini imeanza lini??
(Ila hakunijibu kitu)
Alitoka nje ya ofisi akakutana na wauguzi wanasukuma kitanda alicholazwa angel. Wanakipeleka chumba cha upasuaji. Na yeye alielekea kule kwenye chumba cha upasuaji. Mimi nilisimama nikiwasindikiza kwa macho. Alipofika mbele akiwa kanipa mgongo alisema.
Daktari: Umefanya maamuzi sahihi Olest.
(Nilistuka alivyoniita jina langu)
Daktari aliponigeukia alibadilika kuwa Normak
"Nooooooooooooooooooooooooo" nilipiga kelele hadi nilistuka kutoka usingizini. Nilikuwa nimelala kitandani na ile yote ilikuwa ni ndoto tu. Baada ya ndoto mbaya kama ile niliamua kuamka sikutaka tena kulala. Nilitoka nje, nilipojiangalia kidoleni nilijikuta nimechanjwa kile kile kidole nilichoota nimechanjwa ndotoni. Hapo nilikimbia haraka kurudi hospitali tena. Maana nilihisi kama Angel akifanyiwa upasuaji yawezekana normak akaharibu kila kitu. Nilipo karibia hospitali nilimwona Angel akitoka nje ya hospitali kwa miguu yake na kuingia kwenye gari yao akiwa mzima kabisa.
Nilishangilia kama zuzu nikaamua kurudi nyumbani. Ila nilibaki na mawazo kuhusu dam aliyoichukua Normak ataenda kuifanyia nini?
Usiku ulipofika nilianza kujisikia vibaya nilijiskia kizunguzungu, nilisimama ili niende kujilaza kitandani mara niliona giza totoro nikawa sioni chochote,nilikosa nguv na kuanguka.
Nilistuka kwenye kitanda cha hospitali. Palikuwa na nesi pembeni,nilijiangalia mkononi nilikuwa nimetundikiwa dam. Hapo ndipo nilistuka zaidi. Nilitaka kuamka ila nesi alinizuia.
Nesi: Tulia upo mahali salama tulia.
Aliingia daktari,
Olest: Nipo sawa najisikia vizur, mnaweza kunituhusu tafadhari?? (Sikuyapenda mazingira yale)
Daktari: Hapana umepoteza dam nyingi sana.
Olest: Sinaga tatizo la kuishiwa dam labda tatizo ni nini?
Daktari: Haukuumia labda?
( nikamwonesha kidonda kilichokuwa kidoleni)
Daktari: mmmh.. Hicho kidonda ni kidogo sana,hakiwez kukusababishia upoteze damu nyingi kiasi hicho.
Alianza kuondoka. Alipofika mlangoni nilimsimamisha.
Olest: doctor.... Hujaniambua nini kinaweza kuwa tatizo.
Daktari: kusaini kunaweza kuwa tatizo.
(Nilistuka)
Aliponigeuzia uso alikuwa ni normak. Alitabasam kisha akatoka akabamiza mlango kwa nguvu.
Itaendelea.....
Maoni
Chapisha Maoni